Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In
ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo
mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani.
Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo.Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini.
Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nyuklia.
Michuano ya Olimpiki ya majira ya bariki inatarajiwa kuhusisha pia wanamichezo kutoka Korea Kaskazini jambo ambalo Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In anaeleza kuwa ni la kuimarisha uhusiano zaidi.

No comments:
Post a Comment