Friday, 1 December 2017

Makundi fainali za kombe la dunia nchini urusi.



Kundi A

Kundi hili ndipo alipo mwenyeji wa mashindano haya nchi ya Urusi akiwa
sambamba na Saudi Arabia , Misri na Uruguay. Katika kundi hili Urusi
ndio nchi pekee iliyo chini kisoka katika viwango vya FIFA ikishika
nafasi ya 65 wakifuata Saudi Arabia nafasi ya 63, Misri wanashika nafasi
ya 31 na Uruguay wakiongoza kundi hili kwakuwa nafasi ya 21 katika ubora
wa viwango vya soka duniani. Urusi ana kazi ya ziada kupenya kundi hili
kama nchi mwenyeji kitakwimu ingawa ubora wa FIFA si kigezo sana katika
maandalizi kimbinu na kiufundi kwa maana nzima ya muda mrefu wa
kujiandaa mpaka mwezi juni mwakani. Mechi ya ufunguzi Urusi atakutana na
Saudi Arabia ndio mechi pekee ambayo ana asilimia 50/50 kushinda
ukiangalia ubora wa vikosi vya Uruguay ikiwa na kina Cavan na Suarez
huku Mohamedi Salah akizidi kuonesha ubora wake na Liverpool hivyo
kuingia katika uga wa wachezaji hatari watarajiwao katika fainali za
kombe la dunia nchini Urusi mwakani na kikosi cha mafarao.

Kundi B

Kundi hili ndipo alipo mfalme wa soka kwa sasa duniani Christiano
Ronaldo akiwa na kikosi cha Ureno kitakachofungua mechi za makundi na
Uhispania. Ni fainali za mwisho kwa Ronaldo kutokana na umri wake na
uwezo uwanjani kwa mtazamo wa miaka minne ijayo hivyo inatarajiwa kuwa
makini sana kudhihirishia dunia ubora wake akiwa na kikosi cha Ureno .
Uhispania hawakuwa bora michuano ya mwaka 2014 nchini Brazil hali
iliyowafanya kushindwa kuvuka hatua ya makundi hivyo inaleta changamoto
kwa Ureno , Morocco na Iran . Morocco anahitajika kuwa makini zaidi
ikiwa mara yake ya kwanza kuingia katika michuano hiyo tangu fainali za
mwaka 1998 nchini Ufaransa ili asijegeuka ngazi ya wenzake kusoka mbele.

Kundi C

Ufaransa anapewa nafasi kubwa kupenya kundi hili akiwa na wachezaji
makini na wenye viwango vizuri kama kiungo wa Manchester United Paul
Pogba , Giroud toka Arsenal na Griezman . Wengine kwenye kundi hili ni
Australia, Peru na Denmark. Peru amerudi kwenye michuano hii baada ya
kutoshiriki kwa miaka 38 akipitia njia ya mtoano. Endapo Ufaransa
akizichanga vyema karata zake kuna uwezekano mkubwa wa kuingia hatua ya
16 bora!.

Kundi D

Kama ilivyo kwa kundi B , pia kundi hili lina mfalme mwingine wa soka
Lionel Messi akiwa na kikosi cha Argentina sambamba na nchi za Croatia,
Iceland na Nigeria. Kwa mtazamo wa karibu unaweza kusema Argentina
wakiongozwa na Lionel Messi wanaweza kupita kwa urahisi lakini Iceland
katika kumbukumbu fainali za Euro mwaka 2016 waliweza kumng’oa England
licha ya udogo wao pia hakuna asiyekumbuka maajabu ya Croatia 1998
nchini Ufaransa. Ni kundi gumu kwa maana nzima ya Argentina hivi karibu
kutokuwa na maendeleo mazuri kisoka ngazi ya ushindani. Nigeria hivi
karibuni alicheza mechi ya kirafiki na Argentina na kumfunga 4-2 hivyo
licha ya kupewa nafasi finyu kupenya lakini anaweza kusonga mbele katika
kundi hili pia.

Kundi E

Mabingwa mara tano wa kombe la dunia ‘ the selecao ‘ Brazil yupo kundi
hili akipewa nafasi kubwa kusonga mbele. Serbia , Costa Rica na Uswisi
wana kazi ya ziada kumzuia Brazil kuingia hatua ya 16 bora kutoka kundi
hili. Brazil ndio ilikuwa nchi ya kwanza kufuzu michuano hii na hivi
karibuni chini ya kocha mzawa Tite wamekuwa na kiwango bora sana .
Neymar Jr alishindwa kuipa kikombe Brazil mwaka 2014 hivi sasa
anatarajiwa kuifanyia makubwa nchi hiyo kama key player ili aweze kuwa
katika mizani ya watangulizi wake kama Rivaldo, Cafu, Gaucho , De Lima
na wengineo.

Kundi F

Hili linahesabika kama kundi la kifo likiwa na bingwa mtetezi, Ujerumani
ambaye ameingia hatua hii kwa kishindo baada ya kushinda mechi zote za
kufuzu . Ujerumani yupo na wakali wengine kama Mexico, Sweden na Korea
Kusini. Ni nchi ambazo soka lao linakuwa kwa kasi na wamekuwa na
maandalizi mazuri kuelekea fainali hizi. Ni dhahiri Ujerumani wanapewa
nafasi kupenya kundi hili lakini Mexico sio wakuwabeza waliweza kupenya
hatua ya makundi fainali za mwaka 2014 nchini Brazil, pia Sweden ambao
wamemzuia Italia kushiriki fainali hizi ikiwa ni mara ya kwanza tangia
mwaka 1956!.

Kundi G

Kundi hili linajumuisha nchi za Ubelgiji, watoto wa malikia Elizabeth II
England, Panama na Tunisia. Ubelgiji ndio vinara kisoka katika viwango
vya FIFA katika kundi hili wakishika nafasi ya 5 wakifuatiwa na England
waliopo nafasi ya 15. Tunisia mwakilishi toka Afrika wapo nafasi ya 27
na Panama nafasi ya 56. Kundi hili licha ya Ubelgiji kuwa bora kitakwimu
lakini England wanapewa nafasi kubwa kusonga mbele. Wamekuwa na
maandalizi mazuri kisoka kuliko fainali nyingi zilizopita wakitengeneza
kizazi kipya cha soka cha akina Harry Kane . Meneja wa England wa hivi
sasa Southgate fainali za mwaka 1998 alikuwa mlinzi wa kati wa England
wakiwaadhibu Tunisia hivyo atajipanga vyema kulinda legacy yake na taifa
hilo kwa ujumla.

Kundi H

Lewandowsky akiwa na timu yake ya Poland atakuwa anajaribu kupenya mbele
ya timu zenye uchu wa kufika mbali kisoka katika michuano hiyo. Senegal
walioweza kufika hatua ya robo fainali mwaka 2002 Cisse akiwa mchezaji
na sasa nahodha tayari ameanza kuwapa waafrika matumaini ya kupenya
kundi hilo kwa kiwango kizuri cha timu yake . Colombia na Japan pia ni
mwiba mwingine kwa Poland. Ni kundi ambalo kila timu ina uwezo wa kuvuka
hatua ya makundi endapo itakuwa na maandalizi mazuri.

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers