Thursday, 14 December 2017

Stop unyanyasaji wa wanawake

Nirahisi kumnyanyasa mwanamke ambaye anakutegemea kwa kila kitu, nirahisi kumnyanyasa mwanamke ambaye umemkataza kufanya kazi na kumuambia kubaki kuwa Mama wa nyumbani. Unaweza kumnyanyasa kwakua unajua hawezi kujitegemea, kwamba hata kama akiondoka, hata kama hutawang’ang’ania watoto lakini hawezi kuwalea yeye mwenyewe.
:
.
Unanguvu zote kwakua umemshikilia kikipato, lakini huo si uanaume, wakati mwingine kama umemchoka ni bora kumruhusu aende kuliko kuendelea kumshikilia kama mateka. Kumbuka mwanamke ni kama Paka. Ukimfungia chumbani unaweza kumpiga mpaka ukachoka lakini kama Paka naye akichoka kupigwa na hamna namna ya yeye kutoka chumbani basi anaweza hata kukuua.
:
.
Usifurahie ushindi kwa kupigana na mtu ambaye ushamfanya mnyonge tayari. Maisha si leo tu, kuna kesho ambayo hujui utakua kwenye nafasi gani na wala hujui yeye atakua kwenye nafasi gani? Hata kama moyo wako haumutaki tena, hata kama humfurahii tena kwanini usiongee naye kama binadamu, unapata faida gani kuendelea kumnyanyasa

No comments:

Post a Comment

FIND US ON FACEBOOK

Followers